Maneno: , 1776. Hatujui kama ni kweli, lakini vile tumeambiwa bwana Top­la­dy aliandika maneno haya kama alijificha kutoka upepo kali na mwua, chini ya mwamba, karibu na Ched­dar Gorge kwa Ulaya; Wanasema aliandika maneno haya kwa karatasi kidogo, yaani karata.

Muziki: , 1830.


Mwamba wenye imara,
Kwako nitajificha.
Maji na damu yako,
Toka mbavuni mwako,
Iwe dawa ya kosa,
Kutakasa mioyo.

Si kazi za mikono,
Ziletazo wokovu.
Nikitoa machozi,
Nikifanya kwa bidii,
Siwezi kujiosha,
Unioshe wewe tu.

Sina la mikononi,
Naja msalabani.
Ni uchi, nipe nguo,
Dhaifu, nipe nguvu,
Niondolee taka,
Nitakase sijafa.

Nikaapo dunia,
Nifikapo kifoni.
Nitakapofufuka,
Nitakapokuona,
Mwamba wangu wa kale,
Kwako nitajificha.