Maneno: , before 1901.

Muziki: , 1785 (MI­DI, score).


Yesu, Bin Mariamu,
Bwana wa uzima,
Umefika kwetu
Humu Kanisani.

Kwanza tainama,
Tukukuabudu,
Mungu Mwanadamu
Madhbahuni petu.

Kisha twasujudu
Tukiwaombea
Ndugu zetu pia,
Wale wa kuzimu.

Hawo walukuwa,
Kwanza kama sisi,
Uliwachagua
Wawe watu wako.

Hapa duniani
Walikuungama,
Nawe, Bwana wao,
Usiwasahau.

Walisumbuliwa
Sana na Shetani,
Taabu zimekwisha,
Wape kustarehe.

Kwenye vita kali
Kweli walitiwa
Majeraha mengi,
Bwana, uwaponye.

Upungufu wote,
Doa na nawaa,
Dam yako, Yesu,
Iwaondolee.


Kizungu